Swali: Je, inajuzu kutembea na viatu kwenye makaburi?

Jibu: Kumethibiti kitu ambacho kinatolea dalili ya kuonesha kuwa imechukizwa kufanya hivo katika Hadiyth nzuri. Kulikuwa mtu anayetembelea na viatu makaburini akamwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) avue viatu vyake. Makusudio ni kwamba kutembea na viatu makaburi imechukizwa isipokuwa ikiwa ni kwa haja. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha aliyefanya hivyo kuvivua. Wanachuoni wanasema ni kwa sababu katika kufanya hivyo kuna kuwafanyia khiyana mtu akatembea kati yao na viatu vyake au kwa sababu nyingine ambayo Allaah ndiye Mjuzi zaidi kwayo. Hadiyth hii imezungumziwa [ina kasoro]. Lakini hata hivyo kauli sahihi ni kwamba haina ubaya. Bora zaidi mtu asitembei na viatu isipokuwa ikiwa kama ni kwa haja, kama kwa mfano kuna jua kali au miba. Katika hali hii hakuna neno. Ikiwa hakuna haya mtu asitembee na viatu.

Baadhi ya wanachuoni wengine wameonelea kuwa hakuna ubaya kutembea na viatu. Kwa kuwa imekuja katika Hadiyth Swahiyh ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika maiti husikia nyayo za viatu vya watu wakati wanapoondoka.”

Wakatumia dalili kwa Hadiyth hii kuwa hakuna ubaya kutembea na viatu. Jibu ni kwamba Hadiyth hii haitolea dalili kujuzu kutembea kwa viatu kwenye makaburi. Kwa sababu kutembea kwao huku ni nje ya makaburi. Hakuna kutofautiana kati ya hili na hili. Aula na bora zaidi ni mtu kutotembea na viatu vyake kwenye makaburi isipokuwa kukiwa na haja ya kufanya hivyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=6904
  • Imechapishwa: 05/05/2015