Ibn Baaz kuhusu kuswali nyuma ya Ahl-ul-Bid´ah

Swali: Je, inafaa kuswali nyuma ya mtu ambaye ana ´Aqiydah inayokwenda kinyume na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kama mfano wa Ashaa´irah?

Jibu: Maoni ya sawa – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba kila ambaye tunamuhukumu kuwa ni muislamu basi inasihi kuswali nyuma yake. Vinginevyo itakuwa haifai. Haya ndio maoni ya jopo la wanachuoni na ndio maoni ya sawa.

Ambaye amesema kuwa haijuzu kuswali nyuma ya mtenda dhambi maoni yake ni dhaifu. Dalili ya hilo ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameruhusu kuswali nyuma ya watawala. Kama inavotambulika watawala wengi ni watenda madhambi. Ibn ´Umar, Anas na kikosi cha Maswahabah wengine waliswali nyuma ya al-Hajjaaj ambaye ni miongoni mwa watu madhalimu kabisa.

Kwa kifupisha ni kwamba swalah inasihi nyuma ya mzushi ambaye ana Bid´ah zisizomtoa nje ya Uislamu au mtenda dhambi mwenye dhambi zisizomtoa nje ya Uislamu. Lakini hata hivyo inapaswa kumteua mtu wa Sunnah. Vivyo hivyo watu wakikusanyika wanapaswa kumtanguliza mbele yule ambaye ni mbora wao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (05/426)
  • Imechapishwa: 31/01/2021