Ibn Baaz kuhusu kumuomba du´aa maiti

Swali: Wanafunzi wengi wanaelea kuwa shirki ni kuwaomba maiti wakutatulie haja. Ama mtu akiwaomba maiti uombezi na du´aa wanasema kuwa sio shirki kubwa na kwamba badala yake inakuwa Bid´ah.

Jibu: Hapana. Hii ni shirki kubwa. Kwa kuwa hawawezi kumuombea na wala hawamuombei. Wote ni wenye kushughulishwa na matendo yao. Kumuomba du´aa na uombezi ni wakati wa uhai wake. Kwa ajili hii wakati ´Umar na Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walipotaka kuomba mvua hawakumuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) awaombee. Badala yake walimuomba du´aa ´Abbaas na Yaziyd bin Aswad. Ingelikuwa jambo hili limewekwa katika Shari´ah basi wangelimuomba du´aa ya mvua Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumwambia awaombee ilihali yuko ndani ya kaburi lake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 50
  • Imechapishwa: 25/11/2016