Ibn Baaz kuhusu kumuadhini na kumkimia mtoto mchanga

Swali: Vipi kumtolea adhaana kuliani mwa sikio la mtoto na kumkimia kushotoni mwa sikio?

Jibu: Haya yamewekwa katika Shari´ah kwa mujibu w kundi la wanachuoni. Ni jambo limepokelewa katika baadhi ya Hadiyth ambazo katika cheni zake kuna maneno. Muumini akifanya hivo ni vizuri. Kwa sababu ni miongoni mwa Sunnah na mambo ya kujitolea. Katika cheni ya wapokezi kuna mpokezi anayeitwa ´Aaswim bin ´Ubaydillaah bin ´Aaswim bin ´Umar bin al-Khattwaab na ana udhaifu. Lakini ina mapokezi mengine yenye kuitolea ushahidi. Mtume (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam) alimpa jina mwanae ´Ibraahiym` na haikuhifadhiwa kwamba alimtolea adhaana kwenye sikio lake la kulia na kumkimia kwenye sikio lake la kushoto. Kadhalika wale watoto wa Answaar ambao alikuwa akiletewa ili awafanyie Tahniyq na awape majina. Sijaona kuwa aliwatolea adhaana na kuwakimia masikioni. Lakini muumini akifanya hivo kutokana na ile Hadiyth tuliyoashiria hakuna neno. Lakini zinapeana nguvu baadhi kwa zengine. Ni jambo jepesi. Endapo mtu atafanya ni vizuri kutokana na Hadiyth zinazopeana nguvu. Asipofanya  pia hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/7045/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B0%D8%A7%D9%86-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D8%AD%D8%AF%D9%89-%D8%A7%D8%B0%D9%86%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%88%D9%84%D9%88%D8%AF-%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%A7%D9%82%D8%A7%D9%85%D8%A9-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%AE%D8%B1%D9%89
  • Imechapishwa: 14/06/2019