Ibn Baaz kuhusu kufunga siku ya jumamosi


Swali: Je, Hadiyth inayokataza kufunga siku ya jumamosi isipokuwa ile ambayo tumefaradhishiwa ni Swahiyh?

Jibu: Hadiyth iliyotajwa sio Swahiyh kutokana na mgongano na udhaifu wake, kama walivyozindua hilo wanachuoni wengi. Kwa sababu imesihi ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msifunge siku ya ijumaa isipokuwa kwa kufunga pia siku moja kabla au siku moja baada yake.”[1]

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake. Siku ya baada yake ni jumamosi.

Hadiyth iliyoko hapo juu iko wazi kuonyesha kufaa kufunga jumamosi pamoja na ijumaa.

Vilevile imesihi kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba alikuwa akifunga siku ya jumamosi na siku ya jumapili na akisema:

“Siku hizo mbili ni sikukuu za washirikina na mimi napenda kujitofautisha nao.”[2]

Ameipokea an-Nasaa´iy na Ibn Khuzaymah akaisahihisha.

[1] Ahmad (10052) na Ibn Khuzaymah (2154).

[2] Ahmad (26210).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/410-411)
  • Imechapishwa: 09/06/2018