Ibn Baaz kuhusu jina “Hujjat-ul-Islaam”

Swali: Vipi kumwita mwanachuoni jina la “Hujjat-ul-Islaam”?

Jibu: Hakuna neno. Ni katika mlango wa kuitwa kwa ibara. Hoja ya Uislamu maana yake anapotumia hoja na akazungumza kwamba ni mwenye kustahiki na kufaa. Anatoa dalili na akawazindua watu basi yeye ni hoja ya Uislamu kutokana na elimu na fadhilah zake. Hata hivyo hoja ya kihakika ni Qur-aan, Sunnah na maafikiano. Lakini kunasemwa hivo juu ya baadhi ya wanachuoni “Hujjat-ul-Islaam” kwa sababu ya wingi wa elimu zao na kwamba anapozungumza basi anatumiwa kama hoja na kwa sababu yuko na dalili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 19
  • Imechapishwa: 27/02/2019