Ibn Baaz kuhusu Imaam Ahmad kuona kufaa kufanya Tawassul kwa Mtume

Swali: Je, ni sahihi yale yaliyopokelewa kutoka kwa Imaam Ahmad ya kwamba anaona kufaa kufanya Tawassul kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pekee?

Jibu: Anaona hivo. Lakini kilichotangaa kutoka kwake na kutoka kwa wengine ni makatazo. Wanachuoni wengi wanaona kutofaa. Haijalishi kitu hata kama Imaam Ahmad au mwengine anaona kufaa. Hili ni kosa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 40
  • Imechapishwa: 15/06/2019