Ibn Baaz kuhusu hukumu ya kuoga siku ya ijumaa

Swali: Je, josho la siku ya ijumaa ni lazima au imependekezwa?

Jibu: Kuoga siku ya ijumaa ni Sunnah iliyokokotezwa kutokana zile Hadiyth Swahiyh zilizopokelewa juu ya hilo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ikiwa ni pamoja na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kuoga siku ya ijumaa ni wajibu kwa kila aliyebaleghe, asitumie Siwaak na kujitia manukato.”

“Yule atakayeoga kisha akaenda kuswali ijumaa ambapo akaswali yale aliyoandikiwa kisha akanyamaza mpaka imamu akamaliza Khutbah yake kisha akaswali pamoja naye, basi atasamehewa yaliyo kati yake [ijumaa hiyo] na ijumaa nyingine na ukiongezea na siku tatu.”

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake. Katika tamko jengine imekuja:

”Atakayetawadha, akaweka vizuri wudhuu´ wake, kisha akaenda ijumaa, akasikiliza na kunyamaza, basi anasamehewa yaliyoko kati yake [ijumaa huyo] na ijumaa ijayo na ukiongezea na siku tatu. Na yule atakayegusa kokoto basi amefanya upuuzi.”

Zipo Hadiyth nyingi kwenye mlango huo.

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… ni wajibu kwa kila aliyebaleghe… “

Wanazuoni wengi wanaona kuwa maana yake imesisitizwa. Ni kama ambavo waarabu husema:

“Haki yako juu yangu ni wajibu.”

Kinachofahamisha juu ya maana hiyo ni kule (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutosheka kwake na kutawadha kamai livyokuja katika baadhi ya Hadiyth. Vivyo hivyo kujitia manukato, kutumia Siwaak, kuvaa mavazi mazuri kuliko yote na kwenda mapema yote haya ni mambo yaliyokokotezwa na kupendezwa na hakuna chochote katika hayo ambacho ni lazima.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/170)
  • Imechapishwa: 27/08/2021