Swali: Nataraji utanielekeza katika kitabu cha Hadiyth kizuri?

Jibu: Katika vitabu vizuri kwa mwanafunzi ni kitabu “Buluugh-ul-Maraam”. Ni kitabu kizuri na ni chenye faida katika milango ya Ahkaam. Ni kitabu kizuri na chenye faida, “Buluugh-ul-Maraam” cha Haafidhw Ibn Hajar. Hichi tunatoa nasaha kihifadhiwe na khaswa kuzingatia yaliyomo katika Hadiyth ambazo ni Swahiyh. Na kuna Hadiyth ambazo ni dhaifu lakini ni ndogo na kumebainishwa na kutanabahishwa hali zake. Kuna vitabu vingine vizuri ambavyo ni mukhtasari, “Umdat-ul-Hadiyth” cha ´Abd-ul-Ghaniy bin ´Abd-ul-Waahid bin ´Aliy al-Maqdisiy (Rahimahu Allaah). Kuna jumla ya Hadiyth nzuri. Kuna Hadiyth karimu 400 na zaidi kidogo zenye manufaa na faida. Lakini kilicho cha manufaa zaidi ni “Buluugh-ul-Maraam”. Kwa kuwa chenyewe ni chenye faida zaidi na kina Hadiyth nyingi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 01/04/2018