Swali: ´Awwaam wa Shiy´ah, Suufiyyah na wengineo wapachikwe neno la kufuru kwa kuwafuata?

Jibu: Ni wenye kuwafuata. Ikiwa wanaamini kama wanavyoamini basi ni wenye kuwafuata.

Swali: Kuna wanaowatetea Raafidhwah kwa kutokujua madhehebu yao na pindi tunapowanasihi wanasema kuwa sisi tuna ushabiki.

Jibu: Wawekee wazi ´Aqiydah yao. Nasaha sio ushabiki. Muwekee wazi ya kwamba mfano wake ni kama anayemtetea Ibn Abiy Rabiy´ah. Mbainishie ´Aqiydah yao na kwamba wanapetuka mipaka kwa ´Aliy na wanawaomba uokozi watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ndio ´Aqiydah yao. Wao ni kama makafiri wa Quraysh ambao walikua wakiwaomba uokozi maiti, al-´Uzzaa, Manaat, Habl na masanamu mengine waliokuwa wakiyafanyia ´ibaadah kukiwemo kuyaomba na kuyataka uokozi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 85
  • Imechapishwa: 10/12/2016