Swali: Hekima ya adhaana ya kwanza siku ya ijumaa hii leo imeondoka. Je, hivyo itazingatiwa kuwa ni Bid´ah?

Jibu: Sio Bid´ah. Isitoshe hekima haijaondoka. Aliyesema hivi amekosea. Ikiwa watu wa mwanzo katika Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakati mwingine wanaweza kushughulishwa kutokamana na swalah ya ijumaa na wasizunduke nayo, tusemeje kwa hali zetu sisi tulioko hii leo? Je, hivi sisi ni wenye kuzinduka zaidi kuliko wao kwa ajili ya ´ibaadah? Je, sisi ni wenye kuchunga ´ibaadah zaidi kuliko wao? Hata kidogo. Wao ni wenye kuchunga zaidi kuliko sisi na wabora zaidi kuliko sisi. Kama hilo lilifanywa na khaliyfah mwongofu ambaye ni ´Uthmaan kwa ajili ya kuzindua, waliokuja baada ya Maswahabah ni wenye haja zaidi ya uzinduzi wake, wenye kazi nyingi na upumbaaji mwingi zaidi. Kwa hiyo haja haijaondoka. Ni uzinduzi juu ya kwamba ni siku ya ijumaa ili waumini waweze kujiandaa zaidi kuelekea msikitini. Waislamu waliendelea juu ya kitendo hicho kuanzia zama za khaliyfah mwongofu ´Uthmaan mpaka hii leo katika miji na vijiji vingi. Ni mara chache mno utapata mji au kijiji kisichofanya jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdil-´Aziyz bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3993/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B0%D8%A7%D9%86-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D9%88%D9%84-%D9%8A%D9%88%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%AC%D9%85%D8%B9%D8%A9
  • Imechapishwa: 03/04/2020