Tunajua kipote hiki. Ni kipote kilichopotea. Kiongozi wake ni ´Abdullaah al-Habashiy. Anatambulika kupinda na kupotea kwake. Ni lazima kuwakata, kuwakemea na kuwatahadharisha watu kutokamana nao na kuwasikiliza au kuyakubali yale wanayoyasema. Hapana shaka kwamba ambaye anapinga kwamba Allaah yuko juu ya mbingu ni Jahmiy aliyepotea na kafiri ambaye anakadhibisha maneno Yake Allaah:

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ

“Je, mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika? Au mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokutumieni tufani ya mawe basi mtajua vipi maonyo Yangu.”[1]

Isitoshe anakadhibisha Hadiyth mfano wake zilizopokelewa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Yale yaliyotajwa na Ibn Batwutah kwamba Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah alilinganisha kushuka kwa Allaah na kushuka kwake kwenye daraja za mimbari ni jambo lililozuliwa na halina msingi wowote wa kusihi. Vitabu vyote vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah vinakadhibisha jambo hilo.

[1] 67:16-17

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://binbaz.org.sa/mat/2128
  • Imechapishwa: 29/05/2022