Ibn Baaz kufuta uso baada ya kuomba du´aa

Swali: Ni ipi hukumu ya kunyanyua mikono baada ya Tahiyyat-ul-Masjid, Nawaafil na Sunnah za Rawaatib? Ni ipi hukumu ya kufuta uso?

Jibu: Kunyanyua mikono ni miongoni mwa sababu za kuitikiwa. Imepokelewa katika Hadiyth ya kwamba ni miongoni mwa sababu za kuitikiwa. Kwa hiyo akinyanyua mikono yake baada ya swalah ya sunnah au katika nyakati zengine hakuna neno. Lakini hata hivyo asidumu katika hilo. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa ni mwenye kudumu katika hilo. Alikuwa akifanya hivo baadhi ya nyakati.

Ama kuhusu [kunyanyua mikono] baada ya swalah za faradhi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah wake hawakupatapo kufanya hivo. Lakini inatakiwa kufanya hivo baada ya swalah za sunnah kutokana na ujumla wa dalili katika Shari´ah zinazofahamisha kunyanyua mikono wakati wa kuomba du´aa midhali mtu anafanya hivo baadhi ya nyakati. Hapana neno pasi na mtu kudumu na hilo.

Kuhusu kupangusa uso halikuhifadhiwa katika Hadiyth Swahiyh. Hadiyth iliyosimulia hilo kuna udhaifu ndani yake. Hivyo baadhi ya wanachuoni wakaonelea kuwa hapana neno kufanya hivo kwa sababu zinapeana sapoti na nguvu. Kwa hivyo mtu akifuta hapana neno. Lakini lililo bora ni kuacha kufanya hivo. Kwa sababu Hadiyth Swahiyh zilizopokelewa hakuna ndani yake kufuta uso baada ya kuomba du´aa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/44)
  • Imechapishwa: 03/06/2018