Ibn Baaz kufunga baada ya tarehe 15 Sha´baan

Swali: Je, kufunga baada ya tarehe 15 Sha´baan ni haramu au ni jambo limechukziwa tu?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Sha´baan itapofikia nusu yake basi msifunge.”

Ni Hadiyth Swahiyh.  Yule ambaye hakuanza kufunga mwanzoni mwa mwezi basi asifunge baada ya kufika nusu yake kutokana na Hadiyth hii Swahiyh. Vivyo hivyo iwapo atataka kufunga mwishoni mwa mwezi itakuwa ni aula zaidi kutofaa kufanya hivo. Amesema  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Msiitangulizie Ramadhaan kwa kufunga siku moja wala siku mbili isipokuwa mtu ambaye alikuwa akifunga swawm fulani basi aendelee kuifunga.”

Yule ambaye ana mazowea hakuna neno akaendelea. Kwa mfano mtu ana mazowea ya kufunga jumatatu na alkhamisi ni sawa akaendelea. Kadhalika yule ambaye ana mazowea ya kufunga siku moja na anakula siku ya kufuata ni sawa pia akaendelea. Lakini mtu kuanza kufunga baada ya nusu ya Sha´baan kwa ajili ya Sha´baan haifai.

Ama endapo ataanza kufunga tarehe 14 au tarehe 13 hakuna neno. Ni sawa mtu akafunga mwezi mzima au siku zake nyingi. Lakini mwezi mzima ameanza kula kisha ifikapo katikati yake ndipo anaanza. Hili ndilo lililokatazwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/11186/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%8A%D8%A7%D9%85-%D8%A8%D8%B9%D8%AF-%D9%85%D9%86%D8%AA%D8%B5%D9%81-%D8%B4%D8%B9%D8%A8%D8%A7%D9%86
  • Imechapishwa: 20/04/2018