Ibn Baaz imamu kusoma ndani ya msahafu katika Tarawiyh

Swali: Tunaona katika mwezi wa Ramadhaan imamu anashika msahafu na kusoma ndani yake halafu anauweka pembezoni mwake halafu anarudi kusoma tena ndani yake mpaka pale Tarawiyh itapoisha. Vivyo hivyo anafanya hivo katika swalah ya kisimamo cha usiku katika yale masiku kumi ya mwisho ya Ramadhaan.

Jibu: Hapana ubaya wa kusoma kutoka ndani ya msahafu katika kisimamo cha Ramadhaan kutokana na kule kuwasikilizisha maamuma Qur-aan yote kunakopatikana ndani yake. Jengine ni kwa sababu dalili za Kishari´ah kutoka katika Qur-aan na Sunnah zinafahamisha juu ya Shari´ah ya kusoma Qur-aan ndani ya swalah, jambo ambalo linakusanya kusoma kutoka katika msahafu na kimoyo. Isitoshe imethibiti kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ya kwamb alimwamrisha mtumwa wake aliyemwacha huru, Dhakwaan, kuwaswalisha watu katika kisimamo cha usiku ambapo alikuwa akiswali kutoka ndani ya msahafu. Hayo yametajwa na al-Bukhaariy (Rahimahu Allaah) katika “as-Swahiyh” yake hali ya kuiwekea taaliki na kuiazimia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/40)
  • Imechapishwa: 03/06/2018