Ibn Baaz hukumu ya suruwali na kuswali ndani yake

Swali: Hii leo kumeenea mavazi ya kimagharibi na kunaingia vilevile suruwali. Miongoni mwa sifa zake ni kwamba linabana. Ni ipi hukumu ya kuvaa suruwali hii? Ni ipi hukumu ya kuswali ndani yake kwa sababu inaonyesha viungo visivyokuwa kuonekana wakati mtu anaposujudu?

Jibu: Kuvaa suruwali ni kitu kimeenea kati ya watu na limekuwa sio vazi maalum kwa makafiri. Ni vazi lililoenea na kusambaa kwa waislamu na limekuwa kwa maaskari wao. Kwa hiyo hii leo limekuwa sio vazi maalum kwa makafiri. Bali limeenea kati ya waislamu na wengineo. Ni kama mfano wa viatu, kupanda magari na ndege. Vitu hivi ni kwa ajili ya watu wote na sio maalum kwa makafiri.

Lakini inatakiwa iwe pana na sio yenye kubana. Mtu anatakiwa achunge kitu hichi kinachoonyesha uchi, viungo vyake na kinaidhuru swalah yake. Wasimamizi wanatakiwa kuweka kitu kipana na kizuri cha kufunika viungo visivyotakiwa kuonekana na hakionyeshi fomu ya mwili. Kitu ambacho kitamsaidia katika swalah yake, wudhuu´ wake na mengineyo. Kitu cha kubana na kinachoonyesha viungo visivyotakiwa kuonekana hakitakiwi kuvaliwa. Inavyonidhihirikia ni kwamba haijuzu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3693/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%84%D8%A8%D8%B3-%D8%A7%D9%84%D8%A8%D9%86%D8%B7%D9%84%D9%88%D9%86-%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D9%81%D9%8A%D9%87
  • Imechapishwa: 20/03/2020