Swali 208: Harakati za al-Ikhwaan al-Muslimuun zimeingia Saudi Arabia tangu kitambo na wamekuwa ni wenye uchangamfu wa wazi kati ya wanafunzi. Unasemaje juu ya harakati hizi? Zitakutanishwa vipi pamoja na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?

Jibu: Harakati za al-Ikhwaan al-Muslimuun wamezikosoa wanachuoni maalum. Kwani hawana uchangamfu katika kulingania kwenye Tawhiyd ya Allaah, kukemea shirki na Bid´ah. Wana njia maalum. Wanakosolewa kutokuwa na uchangamfu katika kulingania kwenye Tawhiyd ya Allaah na kuelekeza katika ´Aqiydah sahihi waliyomo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

Kwa hiyo inawapasa al-Ikhwaan al-Muslimuun watilie umuhimu Da´wah ya Salafiyyah, kulingania katika Tawhiyd ya Allaah, kukemea shirki kuabudia makaburi, kuwategemea wafu, kuwataka msaada waliyomo ndani ya makaburi kama al-Hasan, al-Husayn, al-Badawiy na wengineo. Ni lazima watilie umuhimu msingi huu ambao ni “hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah” ambao ndio msingi wa dini.  Kitu cha kwanza ambacho Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alilingania kwacho akiwa Makkah ni katika Tawhiyd ya Allaah na katika maana ya shahaadah. Wanachuoni wengi wanawakosoa al-Ikhwaan al-Muslimuun jambo hili. Bi maana kutokuwa kwao na uchangamfu katika kulingania kwenye Tawhiyd ya Allaah, kumtakasia Yeye nia, kukemea yale yaliyozushwa na wajinga kama kuwategemea wafu, kuwataka msaada, kuwawekea nadhiri na kuchinja kwa ajili yao matendo ambayo ni shirki kubwa.

Vivyo hivyo jengine wanalowakosoa kwalo ni kutokutilia umuhimu Sunnah, kufuata Sunnah, kutilia umuhimu Hadiyth tukufu na yale waliyokuwemo Salaf wa Ummah katika hukumu za Kishari´ah. Yako mambo mengi niliyosikia kutoka kwa ndugu wakiwakosoa. Tunamuomba Allaah awawafikishe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 422
  • Imechapishwa: 15/02/2020