Ibn Baaz akisifu jawabu la al-Albaaniy juu ya kiongozi anayehukumu kinyume na Shari´ah

Nimesikiza jawabu lenye faida la muheshimiwa Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy ambalo limeenezwa katika gazeti “al-Muslimuun” ambapo alikuwa akimjibu aliyemuuliza kuhusu kumkufurisha yule mwenye kuhukumu kinyume na yale aliyoteremsha Allaah[1].

Naonaa kuwa ni maneno ya maana ambayo amesibu haki na amefata njia ya waumini. Ndani yake ameweka wazi kwamba haijuzu kwa yeyote kumkufurisha ambaye anahukumu kinyume na yale aliyoteremsha Allaah pasi na kujua kama amehalalisha jambo hili ndani ya moyo wake au hakuhalalisha. Amejengea hoja kwa maneno ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na maneno ya wengineo katika Salaf. Hapana shaka kwamba yale aliyoyataja wakati wa kufasiri maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ

“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.” (al-Maaidah 05:44)

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ

“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu.” (al-Maaidah 05:45)

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ

“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki.” (al-Maaidah 05:47)

ndio ya sawa. Ameweka wazi kwamba ukafiri umegawanyika aina mbili mkubwa na mdogo kama ambavo dhuluma imegawanyika imegawanyika aina mbili dhuluma kubwa na dhuluma ndogo na ufuska umegawanyika aina mbili ufuska mkubwa na ufuska mdogo. Yule mwenye kuonelea kuwa ni halali kuhukumu kinyume na yale aliyoteremsha Allaah kama mfano wa uzinzi, kula ribaa na mambo mengine ya haramu ambayo kuna maafikiano juu ya uharamu wake basi amekufuru ukafiri mkubwa, kufanya dhuluma kubwa na ufuska mkubwa.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/al-albaaniy-kuhusu-mtawala-anayeweka-hukumu-zilizotungwa-na-watu-badala-ya-shariah/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fitnat-ut-Takfiyr, uk. 54-55
  • Imechapishwa: 28/06/2021