Ibn ´Abdil-Wahhaab Anawakufurisha Waislamu?


Mimi sionelei kuwa ni kafiri yule ambaye anazingatiwa mbele ya Allaah ni muislamu kama ambavyo sionelei vilevile ni muislamu yule ambaye anazingatiwa mbele ya Allaah ni kafiri. Naonelea kuwa ni kafiri yule ambaye mbele Yake anazingatiwa ni kafiri. Yale yaliyosihi kutoka kwa wanachuoni ya kwamba muislamu hawi kafiri yanatakiwa kufasiriwa pale ambapo Bid´ah zake zitakuwa si zenye kukufurisha. Wameafikiana wote kumkafirisha yule ambaye Bid´ah zake zinapelekea katika ukafiri. Ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba ni ukafiri kumkadhibisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika yale yaliyothibiti kwa kukata kabisa. Kutoyajua mambo kama hayo sio udhuru – na Allaah ndiye anajua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaa ar-Raafidhwah, uk. 64
  • Imechapishwa: 16/04/2017