al-Khaliyliy amesema:

“Kuhusu dalili za kinakili – za wanaopinga kuonekana kwa Allaah – baadhi zinapatikana katika Qur-aan na zingine katika Sunnah.”[1]

Kisha akasema:

“Katika Qur-aan ni maneno Yake (Ta´ala):

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ

“Macho hayamzunguki na Yeye ndiye anayazunguka macho yote.”[2]

Halafu akasema:

“Dalili hapa ni kwamba (Ta´ala) amejisifu kuwa macho hayamdiriki. Kudiriki maana yake ni kuona. Ikapata kubainika kuwa kutoonekana kwa macho ni sifa ya kidhati yenye kulazimiana Naye (Ta´ala). Lau kungelikuwa kipindi anaonekana basi kujisifu Kwake kungeondoka na mambo yakishakuwa hivo inageuka kuwa kinyume chake ambacho ni kulaumika – Allaah ametakasika na hilo.”

Akaendelea kusema:

“Kwa upande mwingine ni kwamba [hapa] Allaah anaelezea sifa miongoni mwa sifa Zake na maelezo ya Allaah hayabadiliki. Lau ingelibadilika basi kubadilika kwake ingelikuwa ni kumkadhibisha:

وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ قِيلًا

“Na nani aliye mkweli zaidi kwa kauli kuliko Allaah?”[3]

Wacha nikupe maneno ya wahakiki walivyoifasiri Aayah katika mambo yafuatayo:

Mosi: Kubainisha kuwa katika makanusho matupu hakuna matapo ndani yake, kama anavyoonelea al-Khaliyliy.

Pili: Kubainisha tofauti kati ya “kudiriki” na “kuona”.

Kuhusu tafsiri ya Aayah tumeshatangulia kunukuu kutoka katika Tafsiyr ya Ibn Jariyr kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliyefasiri:

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ

“Macho hayamzunguki na Yeye ndiye anayazunguka macho yote.”[4]

“Macho hayamzunguki.”

Qataadah amesema:

“Ni mkubwa zaidi kwa macho kuweza kumzunguka.”

´Atwiyyah al-´Awfiy amesema:

“Watamtazama Allaah na macho yao hayatoweza kumzunguka kutokana na ukubwa Wake. Lakini Yeye macho Yake yanawazunguka.” Hiyo ndio maana ya maneno Yake:

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ

“Macho hayamzunguki na Yeye ndiye anayazunguka macho yote.”[5]

Kuhusu makanusho matupu hakuna matapo ndani yake tofauti na anavyoonelea al-Khaliyliy na maimamu wake Jahmiyyah, Mu´tazilah na Imaamiyyah katika mlango huu.

[1] Uk. 68

[2] 06:103

[3] 04:122

[4] 06:103

[5] 06:103

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 99-100
  • Imechapishwa: 14/01/2017