Swali: Je, Ibliys ni katika majini au Malaika?

Jibu: Ibliys ni katika majini na sio katika Malaika. Amesema (Ta´ala):

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ الْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِ

“Pindi Tulipowaambia Malaika: “Msujudieni Aadam.” Wakasujudu wote isipokuwa Ibliys alikuwa miongoni mwa majini akaasi amri ya Mola wake.” (18:50)

وَخَلَقَ الْجَانَّ مِن مَّارِجٍ مِّن نَّارٍ

“Akaumba jini kutokana na mwako wa moto.” (55:15)

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Malaika wameumbwa kutokamana na nuru, Ibliys ameumbwa kutokamana na ulimi wa moto na Aadam ameumbwa kwa kile mlichoelezwa.”

Ameipokea Muslim.

Hasan al-Baswriy amesema:

“Ibliys hakuwa katika Malaika kabisa. Asli yake ni jini kama jinsi Aadam (´alayhis-Salaam) asli yake ni mwanaadamu.”

Ameipokea Ibn Jariyr kwa mlolongo wa wapokezi kutoka kwake.

Lakini hata hivyo Ibliys alisaliti maumbile. Hilo lilikuwa pale alipokuwa pamoja na Malaika, akajishabihisha nao, akaabudu na kutekeleza ´ibaadah za Hajj pamoja nao. Kwa ajili hiyo ndio maana aliingia katika kuzungumzishwa na wao na akawa ameasi kwa kwenda kinyume na maamrisho ya Allaah ya kusujudu.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/371)
  • Imechapishwa: 23/08/2020