Ibaadhiyyah wanaafikiana na Jahmiyyah katika kuifasiri imani

5- Maana ya imani kwa mujibu wa Ibaadhiyyah

Ibaadhiyyah pindi walipokuwa wanaelezea nini maana ya imani wamesema yafuatayo: Imani ni kusadikisha kwa moyo kwa kuwa Qur-aan imeweka wazi kwa kuiegemeza imani na moyo… Mja anapoihakikisha imani ndani ya moyo wake na ikakita ndani ya nafsi yake basi anahama na kwenda katika ngazi ya juu zaidi kuliko aliyomo sasa. Nayo ni ngazi ya yakini[1].

Haya ndio maoni ya Jahmiyyah[2] na vifaranga vyao kama Ashaa´irah.

Kuhusu Ahl-us-Sunnah wanaonelea kuwa imani ni kuamini ndani ya moyo, kutamka kwa ulimi na matendo ya viungo vya mwili. Inazidi na inashuka.

[1] Manhaj-ut-Twaalibiyn wa balaagh-ir-Raaghibiyn fiy Usuwl-il-´Aqaaid al-Islaamiyyah (01/69).

[2] Tazama https://firqatunnajia.com/mtazamo-wa-jahmiyyah-juu-ya-imani/

  • Mhusika: ´Abdullaah as-Salafiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ibaadhwiyyah fiy miyzaan Ahl-is-Sunnah, uk. 20
  • Imechapishwa: 18/02/2017