al-Khaliyliy amesema:

“Wamechagua maoni ya kuonekana Allaah (Ta´ala) kuwa muhali wenzetu Ibaadhiyyah. Vilevile ndio maoni ya Mu´tazilah, Jahmiyyah, Zaydiyyah na Shiy´ah al-Imaamiyyah.”[1]

Ole wako, ewe al-Khaliyliy, kwa wale uliojinasibisha nao na kujifakharisha na ´Aqiydah yao. al-Jahm bin Swafwaan na wale waliofuata ´Aqiydah na fikira zake kweli wanaumia kwa kugawanyika kwa Ummah?

Kwa kutumia fursa nitakupa dondoo, mpenzi msomaji unayependa haki na kuinusuru Sunnah, za historia na maisha ya al-Jahm bin Swafwaan ambaye al-Khaliyliy huyu anajifakharisha kwa ´Aqiydah na fikira zake. Hapo ndipo utajua kweli kuwa ndege huruka na wanaofanana naye. Imaam adh-Dhahabiy amesema:

“al-Jahm bin Swafwaan bin Muhriz as-Samarqandiy ni mpotevu, mzushi na ndiye kiongozi wa Jahmiyyah. Alikufa katika zama za Taabi´uun wadogo. Hatujui kuwa alipokea kitu. Lakini hata hivyo alipanda uovu mkubwa.

Baadhi ya sifa zake ni zifuatazo:

1 – Amekanusha Allaah (´Azza wa Jall) kuwa na jina au sifa yoyote.

2 – Kwamba viumbe wametenzwa nguvu.

3 – Qur-aan imeumbwa.

Vilevile ana fikira zingine zilizopinda. Alifariki 128.”[2]

Ibn Athiyr amesema pindi alipokuwa akimzungumzia al-Jahm bin Swafwaan:

“Maoni yake ya kukanusha sifa za Allaah aliyachukua kutoka kwa al-Ja´d bin Dirham, ambaye na yeye alichukua ukanushaji huu kutoka kwa Abaan bin Sam´aan, ambaye na yeye aliyachukua kutoka kwa Twaaluut, ambaye na yeye aliyachukua kutoka kwa mjomba wake Labiyd bin A´swam myahudi ambaye alimfanyia uchawi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Labiyd alikuwa ni zindiki ambaye anasema kuwa Tawraat imeumbwa.”[3]

Huu ndio mlolongo wa Jahmiyyah na Ibaadhiyyah kwa maoni yao kwamba Qur-aan imeumbwa na ndio vilevile mlolongo wa Jahmiyyah wenye kukanusha sifa za Allaah. Hivi kweli yule anayechukua ´Aqiydah yake kutoka kwa Jahmiyyah anaweza kuleta umoja?

Ndugu msomaji hajui anachokusudia anaposema “kuleta umoja wa waislamu”. Anataka kuleta umoja juu ya ´Aqiydah za Jahmiyyah, Mu´tazilah na Imaamiyyah ambao yeye ameongezea juu ya ´Aqiydah zao kukanusha sifa na majina ya Allaah na kuwakufurisha Maswahabah? Au anataka kuleta umoja juu ya ´Aqiydah za Ibaadhiyyah ambao katika mlango wa majina na sifa za Allaah wanaafikiana na Jahmiyyah na inapokuja kwa Maswahabah wao ni Nawaaswib kwa kuwa wamemjengea uadui ´Aliy bin Abiy Twaalib na watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wamewafanya Maswahabah ambao Allaah amesema kuwa ni waadilifu ya kwamba ni kama watu wengine ambao zinawagusa kanuni za Jarh na Ta´diyl. Aidha vilevile wanawahukumu waislamu waliokufa katika dhambi kubwa kwamba watadumishwa Motoni milele huko Aakhirah. Haya yametajwa na mwandishi katika kitabu chake hichi ambacho sisi tuko tunakikosoa na kukijadili. Njama ovu haziwazunguki isipokuwa wenye nazo wenyewe.

[1] Uk. 32

[2] Miyzaan-ul-I´tidaal (01/441)

[3] al-Kaamil (07/75)

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 37-39
  • Imechapishwa: 14/01/2017