Ibaadhiyyah hawatomuona Allaah Aakhirah


al-Khaliyliy amesema kuwa amesikia muhadhara uliyorekodiwa kwenye mkanda kutoka kwa Khatwiyb mmoja hivi anayejulikana katika nchi moja ya kisiwa cha kiarabu akitumia maneno Yake (Ta´ala):

كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ

“Sivyo hivyo! Hakika wao siku hiyo bila shaka watazuiwa kumuona Mola wao.”[1]

na kwamba miongoni mwa aliyoyasema ni kuwa Ibaadhiyyah watazuiwa kumuona Mola wao pindi waumini watapomuona[2].

Kuhusu mimi sijasikia mkanda huu. Lakini hata hivyo napenda kumuuliza ni kwa nini anaathirika kwa hilo ilihali yeye ndiye mwenye kukanusha kuonekana Allaah (Ta´ala) na kwamba hakuna atayemuona na anasema vilevile kwamba hiyo ndio ´Aqiydah ya Ibaadhiyyah na ametunga kitabu kutilia hilo nguvu?

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wao wanaamini yale aliyoelezea Allaah (Ta´ala) katika Kitabu Chake ya kwamba waumini watamuona Mola wao siku ya Qiyaamah na vilevile wanaamini yale Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba waumini watamuona Mola wao.

Dalili zimefahamisha kuwa mtu analipwa sawa na vile alivyotenda. Waumini kumuona Mola wao Aakhirah ni kutokana na vile walivyotenda. Inahusiana na uoni kumfikia Mola wao pindi watapokuwa Peponi.

Ibaadhiyyah pia watalipwa sawa na vile walivyotenda. Kwa vile wamepinga kuonekana kwa Allaah [Aakhirah] na wakazirudisha dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah zinazofahamisha hivo, kunyimwa hilo ni malipo yanayoafikiana nao na Mola hamdhulumu yeyote. Mimi naona kuwa Khatwiyb anayelaumiwa hakutaja isipokuwa kitu ambacho mwandishi amejichagulia mwenyewe na kile kilichochaguliwa na kipote chake Ibaadhiyyah. Kwa nini basi alaumu kwamba Khatwiyb huyo ndiye ambaye amesema:

“Ibaadhiyyah ndio ambao watazuiwa kumuona Mola wao siku ya Qiyaamah”?

Hakuna alichofanya Khatwiyb huyu isipokuwa ametaja kile ambacho Ibaadhiyyah wamejichagulia Kishari´ah na kimfumo. Khatwiyb hajasema kitu kutoka kwake mwenyewe. Dalili ya hilo ni kwamba mwandishi – yaani al-Khaliyliy – amesema katika ukurasa wa 32:

“Wenzetu Ibaadhiyyah wamechagua maoni ya kuonekana Allaah (Ta´ala) – duniani na Aakhirah – ya kwamba ni muhali. Vilevile ndio maoni ya Mu´tazilah, Jahmiyyah, Zaydiyyah na Shiy´ah al-Imaamiyyah.”

[1] 83:15

[2] Uk. 30

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 58
  • Imechapishwa: 14/01/2017