Ibaadhiyyah Ahl-ul-Haqq wal-Istiqaamah?


Ikiwa mwandishi, al-Khaliyliy, anasema kuwa kipote chake ndicho Ahl-ul-Haqq wal-Istiqaamah na kwamba hawakuchukua ´Aqiydah yao isipokuwa kutoka katika Qur-aan na Sunnah, tunamwambia yafuatayo:

Haki na msimamo ni kuchukua yale yaliyokuja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na si kuyarudisha kwa kufuata matamanio, upotoshaji wa kukusudia na kutangulia mbele ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 92
  • Imechapishwa: 14/01/2017