´Ibaadah za ambaye hajatahiriwa zinakubalika?

Swali: Inajuzu kwa muislamu ambaye kishabaleghe na yuko na akili anafunga na kuswali ilihali si msafi hajatahiriwa? Ni ipi hukumu ya mwenye kuacha kutahiriwa?

Jibu: Ikiwa haogopi madhara ya kutahiriwa basi ni lazima kwake kutahiriwa. Kwani hilo ni jambo limewekwa katika Shari´ah na limekokotezwa kwa maafikiano ya maimamu. ash-Shaafi´iy na Ahmad, kama inavyojulikana, wanaonelea kuwa ni wajibu. Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitahiriwa baada ya miaka thamanini. Wanatakiwa kuendewa madaktari waaminifu kukikhofiwa madhara. Ikiwa kutahiriwa kunamdhuru katika majira ya joto basi acheleweshe mpaka kunako majira ya baridi. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/113-114)
  • Imechapishwa: 19/11/2017