´Ibaadah kwa ziada usiku wa tarehe 27 Ramadhaan

Swali: Baadhi ya watu wanalenga usiku wa tarehe ishirini na saba kuwafuturisha wafungaji msikitini, kutoa zakaah na kufanya ´Umrah kiasi cha kwamba katika usiku huo kunatokea msongamano mkubwa kabisa.

Jibu: Malengesho yote haya yanakwenda kinyume na nia na Sunnah. Sunnah ni kutolengesha ´Umrah katika usiku wa tarehe ishirini na saba. Ramadhaan nzima ni ya kufanya ´Umrah, ni mamoja usiku au mchana. Ramadhaan nzima ni wakati wa kutoa zakaah. Yule anayetaka kutoa swadaqah anaweza kutoa katika Ramadhaan au nje ya Ramadhaan.

Kuhusu usiku wa tarehe ishirini na saba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa salam) amesema juu yake:

”Yule atakayesimama kuswali usiku wa Qadr kwa imani na kwa matarajio, basi atasamehewa dhambi zake zilizotangulia. Usiku wake wenye matarajio makubwa ni tarehe ishirini na saba.”

Amesema ”Yule atakayesimama kuswali”. Hakusema ”Yule atakayefanya ´Umrah wala kwamba yule atakayetoa swadaqah au kwamba yule atakayetoa zakaah ya mali yake”. Amesema:

”Yule atakayesimama kuswali usiku wa Qadr kwa imani na kwa matarajio, basi atasamehewa dhambi zake zilizotangulia.”

Unakuwa katika zile siku kumi za mwisho za Ramadhaan. Usiku wake wenye matarajio makubwa ni zile nyusiku za witiri ambazo ni usiku wa tarehe ishirini na moja, ishirini na tatu, ishirini na tano, ishirini na saba au ishirini na tisa. Usiku wenye matarajio makubwa katika nyusiku hizi ni usiku wa tarehe ishirini na saba. Lakini maoni yenye nguvu zaidi ni kwamba ni wenye kuhamahama. Mwaka mmoja unaweza kuwa katika usiku wa tarehe fulani, mwaka mwingine katika usiku wa tarehe nyingine. Ni usiku wenye kuhamahama. Kama ambavo pia unaweza kutokea katika nyusiku ni nyusiku za shufwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=8qhLiOxaLkU
  • Imechapishwa: 15/05/2020