´Ibaadah kwa mwanamke ambaye nifasi yake imeendelea zaidi ya siku arobaini

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kufunga kabla ya kukamilisha siku arobaini damu ikimsimama au anapaswa kukamilisha siku arobaini?

Jibu: Pale tu ataposafika basi ni lazima kwake kufunga na kuswali ingawa atakuwa ndani ya asiku arobaini. Kipindi hicho atakuwa ni halali kwa mume wake. Kinachozingatiwa ni kusafika. Akisafika chini ya siku ishirini, au thelathini basi ataoga na baadaye ataswali, atafunga na kuhalalika kwa mume wake ijapo hayajakamilika masiku arobaini.

Damu ikimwendelea zaidi ya siku arobaini basi atatakiwa kuoga ile siku ya arobaini hata kama atakuwa na damu. Kwa sababu kikomo chake ni arobaini. Hivyo atatakiwa kuoga, kuswali na kufunga na atakuwa ni halali kwa mume wake baada ya asiku arobaini ijapo atakuwa na damu. Hata hivyo atatakiwa kutawadha kipindi cha kila swalah na kujihifadhi kwa pamba au kitu mfano wake ili  isimame. Isipokuwa ikiwa kama damu hiyo ya uzazi itakutana na wakati wa hedhi. Kipindi hicho cha hedhi atatakiwa kukaa midhali yatazidi masiku arobaini.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4422/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B7%D9%87%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D9%86%D9%81%D8%B3%D8%A7%D8%A1-%D9%82%D8%A8%D9%84-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B1%D8%A8%D8%B9%D9%8A%D9%86-%D9%88%D8%AA%D8%A7%D8%AE%D8%B1%D9%87-%D8%A8%D8%B9%D8%AF%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 12/09/2020