Swali: Ni ipi hukumu ya swawm ya mwenye kuacha swalah?

Jibu: Mwenye kuacha swalah swawm yake sio sahihi na wala haikubaliwi kutoka kwake. Kwa kuwa mwenye kuacha swalah ni kafiri na ni mwenye kuritadi. Amesema (Ta?ala):

“Wakitubu na wakasimamisha swalah? na wakatoa zakaah, basi ni ndugu zenu katika dini. Tunazipambanua Aayah kwa watu wanaojua.” (09:11)

Mtume (Swalla Allaahu ?alayhi wa sallam) amesema:

“Baina ya mtu na ukafiri na shirki ni kuacha swalah.”

“Ahadi iliyopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi yule mwenye kuiacha amekufuru.”

Haya ndio maoni ya Maswahabah wengi ikiwa hawakuafikiana juu ya hili. ?Abdullaah bin Shaqiyq (Rahimahu Allaah), ambaye ni mmoja katika Taabi?uun wenye kujulikana, amesema:

“Hakuna kitu Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ?alayhi wa sallam) walikuwa wakionelea kukiacha ni ukafiri kuliko swalah.”

Kujengea juu ya hili mtu akifunga ilihali haswali basi swawm yake ni yenye kurudishwa na si yenye kukubaliwa. Jengine ni kwamba haitomfaa kitu mbele ya Allaah siku ya Qiyaamah. Sisi tunamwambia: anza kuswali kwanza kisha ndio ufunge. Ama kufunga ilihali hauswali, swama yako ni yenye kurudishwa. Ibaadah za kafiri hazikubaliwi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/87-88)
  • Imechapishwa: 29/05/2017