Swali: Inajuzu kutumia kama dalili fatwa ya mwanachuoni miongoni mwa wanachuoni wanaosema kuwa adhaana ya ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) siku ya Ijumaa baada ya zama za Maswahabah inazingatiwa kuwa ni Bid´ah?

Jibu: Huyu sio mwanachuoni. Mwenye kusema kuwa adhaana ya kwanza ambayo iliamrishwa na ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye alikuwa khaliyfah watatu mwongofu – isitoshe aliiamrisha katika zama za Muhaajiruun na Answaar na hawakumkemea – mtu huyu sio mwanachuoni katika mambo haya. Haijalishi kitu hata kama anaweza kuwa ni msomi katika mambo mengine. Lakini inapokuja katika mambo haya ni mjinga.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=KPdm-HBJBC4
  • Imechapishwa: 03/07/2018