Swali: Ni nini maana ya kushuhudia ya kwamba hapana mungu mwenye kuabuduiwa isipokuwa Allaah? Je, inamtosheleza mtu kuingia katika Uislamu au kuna matendo mengine yanayoilazimu yanayompelekea yule mwenye kuisema kuwa muislamu? Ni ipi tofauti kati ya muislamu na muumini?

Jibu: Kushudia ya kwamba hapana mungu mwenye kuabuduiwa isipokuwa Allaah maana yake ni kutambua na kukubali kwa moyo na kutamka kwa ulimi ya kwamba hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Inatosha kumwingiza mtu katika Uislamu kwa sharti akijua maana yake na ukayafanyia kazi muqtadha yake. Ama ikiwa hatendei kazi muqtadha yake; akawa haswali, hafungi na wakati huohuo anasema ya kwamba hapana mungu mwenye kuabuduiwa kwa haki isipokuwa Allaah, lakini hata hivyo akawa haswali, hafungi na wala hatekelezi nguzo za Kiislamu sio muislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/node/16570
  • Imechapishwa: 07/05/2017