Huyu sio mke, taliki haraka iwezekanavyo!


Swali: Muulizaji kutoka Ufaransa anasema “Nilioa mwanamke na sote tulikuwa na watoto wadogo. Na baada ya hapo nikaja kujua kuwa mke wangu anatumia madawa ya kulevya. Ipi nasaha yako na je inajuzu kwangu kumtaliki kwa sababu hii”?

Jibu: Si kwamba inajuzu, bali ni wajibu kwako kumtaliki maadamu anatumia madawa ya kulevya. Huyu anaiharibu nyumba yako na watoto wako. Wewe unamuhifadhi naye ni mujrima. Ni wajibu kwako kufanya haraka kumtaliki na kuachana nae. Isipokuwa tu ikiwa ametubu Tawbah iliokuwa ya kweli na kuacha madawa ya kulevya, hapo atakuwa mke wako. Ama akiendelea, haistahiki kubaki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/10038
  • Imechapishwa: 04/03/2018