Swali: Ni lini asiyekuwa mwarabu anakuwa ni mbora kuliko mwarabu?

Jibu: Hukumu katika hilo ni kama alivyozindua Allaah (Subhaanah) pale aliposema:

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ

“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana mwanamme na mwanamke na tukakufanyeni mataifa na makabila ili mtambuane. Hakika mtukufu zaidi miongoni mwenu mbele ya Allaah ni yule mwenye kumcha Allaah zaidi.”[1]

Asiyekuwa mwarabu akiwa ni mwenye kumcha Allaah zaidi basi yeye ndiye mbora. Kinyume chake mwarabu akiwa ndiye mwenye kumcha Allaah zaidi basi yeye ndiye mbora. Ubora, utukufu na hadhi inategemea na kumcha Allaah. Yule ambaye atakuwa ni mwenye kumcha Allaah zaidi yeye ndiye mbora. Ni mamoja ni mwajemi au mwarabu.

[1] 49:13

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (05/355) https://binbaz.org.sa/fatwas/1290/%D9%85%D8%AA%D9%89-%D9%8A%D9%83%D9%88%D9%86-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B9%D8%AC%D9%85%D9%8A-%D8%A7%D9%81%D8%B6%D9%84-%D9%85%D9%86-%D8%A7%D9%84%D8%B9%D8%B1%D8%A8%D9%8A
  • Imechapishwa: 16/01/2020