Huyu ndiye mbora zaidi mbele ya Allaah


Swali: Ni lini asiyekuwa mwarabu anakuwa mbora kuliko mwarabu?

Jibu: Hukumu katika hilo, ni kama alivyozindua Allaah (Subhaanah) pale aliposema:

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا

“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamme na mwanamke na tukakufanyeni kuwa mataifa na makabila ili mtambuane. Hakika aliye mbora zaidi miongoni mwenu mbele ya Allaah ni yule mwenye taqwa zaidi kati yenu.”[1]

Asiyekuwa mwarabu akiwa yeye ndiye mwenye kumcha Allaah zaidi basi yeye ndiye bora. Vivyo hivyo mwarabu akiwa yeye ndiye mwenye kumcha Allaah zaidi basi yeye ndiye bora. Ubora, heshima na nafasi inategemea na uchaji Allaah. Ambaye anamcha Allaah zaidi basi yeye ndiye mbora. Ni mamoja si mwarabu au ni mwarabu.

[1] 49:13

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (05/355)
  • Imechapishwa: 12/02/2021