Huyu ndiye Mahram anayekubalika Kishari´ah

Swali: Miongoni mwa masharti ya Mahram anayesafiri na mwanamke ni lazima awe amekwishabaleghe?

Jibu: Ndio. Miongoni mwa masharti ya Mahram ni lazima awe ameshabaleghe na ni mwenye akili. Ikiwa bado hajabaleghe malengo hayatofikiwa. Malengo ya Mahram ni yeye kumtetea mwanamke. Ni lazima pia awe ni mwenye akili na mtambuzi wa kile kinachozungumzwa. Akiwa ni mtoto asiyefahamu mwanamke anaweza kuzungumza maneno na mwanaume asiyekuwa Mahram wake ambapo mwanamke huyo akampa ahadi na mengineyo na huku mtoto huyu asijue kitu na asiweze kufanya kitu. Katika hali hii Mahram atakuwa hana faida yoyote. Malengo ya Mahram ni yeye kumlinda na kumtetea mwanamke kutokamana na mwanaume ambaye si Mahram wake. Akiwa bado ni mtoto hawezi kuathiri kitu. Mwanamke huyo na mwanaume wanaweza kukubaliana mambo na kutongozana na mtoto huyu asiyejue kitu. Kadhalika mtoto huyu endapo kutahitajika kumtetea hawezi kufanya hivo. Kwa hiyo ni lazima Mahram awe ameshabaleghe na mwenye akili na kukomaa ambaye anaelewa. Hata kama ameshabaleghe lakini haelewi kitu haisaidii kitu. Ni lazima awe mkomavu na mwenye kuelewa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa//index.cfm?do=cms.AudioDetails&audioid=63283&audiotype=lectures&browseby=speaker
  • Imechapishwa: 16/09/2017