Huyu ndiye anafaa kufanya Da´wah


Swali: Je, inajuzu kwa mtu yeyote kuamrisha mema na kukataza maovu?

Jibu: Hapana. Yule ambaye yuko na elimu ndiye ambaye anatakiwa kuamrisha mema na kukataza maovu. Anapaswa kuwa na elimu ya ni yepi mema na ni yepi maovu. Kuna uwezekano mjinga akaamrisha maovu na akakataza mema kwa sababu ya ujinga. Ni lazima awe na utambuzi:

قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ

“Sema: “Hii ndio njia yangu nalingania kwa Allaah juu ya ujuzu.” (12:108)

Mwenye kuamrisha mema na kukataza maovu ni lazima awe na maarifa na elimu. Vinginevyo ataharibu zaidi kuliko atavyotengeneza. Hali kadhalika walinganizi katika dini ya Allaah; ni lazima wawe na elimu juu ya yale wanayolingania kwayo. Vinginevyo wataharibu zaidi kuliko wanavyotengeneza. Ndio maana idara ya kidini inaajiri tu watu walio na elimu na utambuzi wa mambo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (21) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1434-08-14.mp3
  • Imechapishwa: 22/05/2018