Swali: Kuna ambao wanadhani kuwa kukataza kwa moyo kunatosheleza kutokataza kwa ulimi. Ni yapi ya sahihi katika hayo?

Jibu: Kukataza kwa moyo kunakuwa kwa yule ambaye hakuweza kukataza kwa mkono na kwa kuzungumza. Hapo angalau kwa uchache ndipo anatakiwa kukataza maovu kwa moyo. Katika hali hiyo anatakiwa kujitenga na sehemu hiyo na awatenge watu wake. Haifai kwake kukaa nao na kuanza kucheka nao na kusema kuwa anachukia kwa moyo wake. Ikiwa kweli unachukia basi usiketi nao:

وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ

”Unapowaona wale wanaojiingiza katika Aayah Zetu, basi jitenge nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka, usikae pamoja na watu madhalimu.”[1]

[1] 6:68

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (81) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-1-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 01/04/2018