Swali: Huluuliyyah ni watu gani?

Jibu: Huluuliyyah ni wale wenye kuitakidi kuwa Allaah amekita kila mahali na kwamba amekita kwenye viumbe Wake. Bahaa-iyyah vilevile wanaonelea hivo. Wanasema kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) amekita kwa kiumbe. Kuna Suufiyyah ambao vilevile wanaitakidi imani hii ya Huluuliyyah. Ni Huluuliyyah wa Suufiyyah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (12) http://alfawzan.af.org.sa/node/2055
  • Imechapishwa: 14/03/2017