Hukumu za Twaaghuut za wazee viongozi wa makabila

Swali: Kati yetu hutokea baadhi ya magomvi na wale wenye kuhasimiana wanaenda kwa baadhi ya viongozi wa makabila ambao wanahukumu kinyume na hukumu ya Allaah. Ni upi usahihi wa hukumu yao? Je, inajuzu kuhukumiwa kwa hayo?

Jibu: Haya ni batili. Hizi ni hukumu za wakati kabla ya kuja Uislamu. Hizi ndio hukumu za Twaaghuut. Haijuzu kuhukumiwa kinyume na Shari´ah takasifu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (83) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-15-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 12/01/2018