Swali: Ni ipi hukumu ya swawm za pamoja kwa njia ya kwamba wanakusanyika kundi la watu na kukubaliana kufunga masiku maalum kama jumatatu na alkhamisi na hilo ni kwa lengo la kusaidia katika wema na uchaji Allaah? Kwa sababu mtu ambaye ni dhaifu kwenye nafsi yake anapata nguvu kupitia nduguze. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Naona kuwa sio katika Sunnah na kwamba ni aina moja wapo ya Bid´ah[1] wakiafikiana juu ya hilo. Ikiwa kwa mfano tunakataza kuleta Takbiyr au Dhikr za pamoja na hii vilevile ni swawm ambayo ni ´ibaadah na hivyo haitakikani iwe kwa pamoja. Lakini ikitokea bila ya kuafikiana haina neno. Kwa mfano imetokea wamefunga [wote] siku ya jumatatu na wakaambizana kwamba yule ambaye amefunga basi futari leo itakuwa kwa fulani na hivyo wakaafikiana juu ya hilo. Katika hali hii haina neno. Kwa sababu ni jambo lililotokea na hawakuafikiana juu ya kufanya ´ibaadah.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/swawm-za-pamoja-jumatatu/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (25)
  • Imechapishwa: 15/01/2019