Hukumu ya swalah ya kupatwa kwa jua na kama inafaa kwa mwanamke kuswali nyumbani kwake

Swali: Ni ipi hukumu mwanamke kuswali swalah ya kupatwa kwa jua nyumbani kwake? Je, inafaa kwa mwanamke kuswali msikitini?

Jibu: Aswali msikitini. Kwa sababu wanawake wa Maswahabah walihudhuria swalah ya kupatwa kwa jua wakati jua lilipopatwa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Inafaa vilevile kwao kuswali majumbani mwao. Maoni yaliyo sahihi zaidi ya wanachuoni ni kwamba swalah ya kupatwa kwa jua ni faradhi kwa baadhi ya watu na kwamba ni lazima swalah ya kupatwa kwa jua iswaliwe nchini. Kwa mfano ikiwa tuko mjini ni lazima kwetu kuswali swalah ya kupatwa kwa jua. Lakini hata hivyo si lazima kwa misikiti yote isipokuwa kwa njia ya mapendekezo.

Bora swalah ya kupatwa kwa jua iswaliwe katika ile misikiti mikubwamikubwa, kama walivyotaja wanachuoni na kama jinsi dhahiri ya Sunnah inafahamisha hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakusanya watu mahala pamoja kisha akawasomea kisomo kinachofahamisha kwamba kisomo hichi ni cha mkusanyiko. Hivyo ni kwa sababu alisoma kwa sauti ya juu ilihali anaswali mchana. Hatutambui kuwa kuna swalah inayosomwa kwa sauti ya juu mchana isipokuwa tu zile swalah ambazo watu wanakusanyika kwazo. Mfano wa swalah hizo ni swalah za ´iyd, swalah ya ijumaa na swalah ya kuomba mvua. Hiyo ikawa ni dalili inayofahamisha kwamba bora waislamu wakusanyike katika ile misikiti mikubwamikubwa. Misikiti hiyo ina haki zaidi ili Khatwiyb aweze kuwakhutubia waswaliji kwa sababu yeye ndiye Khatwiyb wa msikiti. Anatakiwa kuwatolea watu Khutbah baada ya kumaliza kuswali swalah ya kupatwa kwa jua.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (72) http://binothaimeen.net/content/1657
  • Imechapishwa: 07/04/2020