Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya ´Iyd? Je, mtu anailipa ikimpita?

Jibu: Kilicho dhahiri ni kwamba swalah ya ´Iyd ni faradhi kwa kila mmoja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameiamrisha. Ikimpita mtu basi hailipi. Jambo la kuilipa halikuthibiti. Hilo ni tofauti na swalah ya ijumaa. Swalah ya ijumaa ikimpita mtu anatakiwa kuilipa. Lakini hata hivo hatumwambii alipe swalah ileile, badala yake tunamwambia aswali Dhuhr.  Hilo ni kwa sababu wakati huu ni ima ijumaa au Dhuhr. Hivyo ijumaa ikimpita badala yake aswali Dhuhr.

Kuhusu swalah ya ´Iyd imewekwa katika Shari´ah kwa njia ya mkusanyiko. Akipata mkusanyiko huu aswali. Asipopata mkusanyiko huu asilipe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawa (16/214)
  • Imechapishwa: 14/06/2018