Hukumu ya ndoa za muda kwa wale wanaosafiri kwenda miji ya nje


Swali: Ipi hukumu ya kuoa kwa nia ya Talaka kwa mwenye kusafiri au kuishi mwezi au miezi miwili katika mji mwingine?

Jibu: Hili halijuzu. Kuoa kwa nia ya Talaka haijuzu kwa kuwa inashabihiana na Mut´ah. Aoe kwa nia ya kudumu nae. Akiwa mwema adumu nae na kama hakuwa mwema amtaliki. Ama kuoa kwa nia ya Talaka baada ya wakati fulani, hii ndio Mut´ah. Ipi tofauti ya hili na Mut´ah?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/12880
  • Imechapishwa: 05/03/2018