Hukumu ya ndoa ya makafiri wanaosilimu pamoja


Swali: Mtu akisilimu na mke wake ilihali ni Mulhiduun (makafiri) au waabudu masanamu, je, atabaki kuwa ni mke wake au amtaliki?

Jibu: Mke akisilimu anatengana naye. Lakini mume akisilimu ndani ya eda, mke anarudi kwake. Ama eda ikiisha na akawa bado hajasilimu, mwanamke huyu anakuwa amekwishatengana naye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (68) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13864
  • Imechapishwa: 16/11/2014