Swali: Jana tulijifunza ya kwamba yule mwenye kufanyia mzaha Dini ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anakufuru. Je, mwenye kukanusha Hadiyth ya kunywa mkojo wa ngamia, anaifanyia mzaha na anasema kuwa inaenda kinyume na maumbile na usalama anakuwa kafiri?

Jibu: Ndio. Akifikiwa na Hadiyth na akajua kuwa Hadiyth ni Swahiyh haijuzu kwake kuipinga na kupinga kuwa mkojo wa ngamia ni dawa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kuwa mkojo wa ngamia ni dawa ya homa. Ameamrisha yule ambaye ameshikwa na homa kunywa maziwa ya ngamia na mkojo wa ngamia. Ameeleza kuwa mkojo wa ngamia na maziwa ya ngamia ni dawa inayotibu homa. Yule mwenye kumkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na huku anajua kuwa Hadiyth ni Swahiyh anaritadi kutoka katika Dini ya Uislamu. Kwa sababu anamkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/nawaqid-19-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/04/2015