Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke wa Kiislamu kuolewa na mwanaume asiyekuwa muislamu?

Jibu: Haijuzu kwa mwanamke Muislamu kuolewa na asiyekuwa Muislamu moja kwa moja. Haijuzu kwa mwanamke wa Kiislamu kuolewa na kafiri wala mshirikina.

لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

“Wao [wanawake wa kiislamu] si halali kwao [hao makafiri] na wala wao [waume] si halali kwao.” (60:10)

وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ

“Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni.” (02:221)

Mwanamke wa Kiislamu haijuzu kuolewa na kafiri, ni mamoja awe Kitaabiyyah – myahudi au mnaswara – au asiyekuwa Kitaabiyyah. Ama kinyume chake, muislamu akaoa mwanamke wa Kitaabiyyah, hili linajuzu kutokana na andiko la Qur-aan. Kwa kuwa mwanamke anakuwa chini ya utawala wa mwanaume. Kwa ajili hii huenda akasilimu na isitoshe anakuwa chini ya utawala wa mwanaume. Tofauti na mwanaume kafiri akiwa mume wa mwanamke wa Kiislamu, mwanamake huyo anakuwa chini ya utawala wa kafiri na tunaomba kinga kwa Allaah. Kuna khatari akamtoa katika Dini yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13517
  • Imechapishwa: 10/04/2022