Hukumu ya mwanamke kunuia swawm ilihali yuko na hedhi kwa kutarajia atasafika siku hiyo

Swali: Kuna mwanamke siku kadhaa kabla ya Ramadhaan alipata ada yake ya mwezi kisha Ramadhaan ikamwingilia ilihali bado hajatwaharika. Siku ya pili ya Ramadhaan akanuia kufunga na huku anasubiri damu ikatike ilihali ni mwenye kujizuia na chakula na kinywaji anasubiri siku iishe. Damu ilikatika kabla ya jua kuzama na huku ni mwenye kujizuia na chakula na kinywaji siku nzima na bado hajaoga. Je, alipe siku yake hii au hapana?

Jibu: Swawm yake ni haramu kwake. Si halali kwa mwanamke kufunga kabisa ilihali bado yuko na hedhi. Kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Je, pale anapopata hedhi si aswali wala hafungi?”

Hili ni jambo wanachuoni wote (Rahimahum Allaah) wameafikiana.

Kujengea juu ya hili ni wajibu kwa mwanamke huyu kulipa ile siku ya kwanza na siku ya pili na atubu kwa Allaah kwa vile alinuia kufunga ilihali yuko na hedhi.

Ni wajibu kwa mwanamke iwapo atasafika kabla ya Fajr basi aoge na kuswali swalah ya Fajr. Aendelee na swawm yake ijapokuwa hatowahi kujisafisha isipokuwa baada ya alfajiri kuingia. Ni kama mfano iwapo atakuwa na janaba na mtu asiwahi kujisafisha kujisafisha isipokuwa baada ya alfajiri kuingia. Katika hali hii hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1592
  • Imechapishwa: 13/06/2018