Hukumu ya msemo bahati mbaya au nzuri

Swali 252: Je, inafaa kwangu kusema “Kwa bahati mbaya/nzuri nikakutana na fulani” au mfano wa maneno hayo, kusema kwamba “Yakitaka makadirio” au kwamba “Yalitaka makadirio nende sehemu fulani na mfano wa hayo?

Jibu: Anapaswa aseme “Allaah akataka nende sehemu fulani”. Iwapo atasema kwa bahati mbaya/nzuri ilihali haamini kwamba bahati hii inaathiri na kwamba haina athari yoyote katika jambo hili, basi itambulike kuwa ni katika maneno yaliyozoeleka kwenye midomo ya watu. Hayafikii kiwango cha uharamu. Lakini bora zaidi aseme “Allaah akitaka na akikadiria kukutana na fulani”. Aegemeze kitendo kwa Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 471
  • Imechapishwa: 13/03/2020