Hukumu ya msemo أقامها الله وأدامه

Swali: Tunawasikia baadhi ya watu wakisema:

أقامها الله وأدامها

“Allaah aisimamishe na kuidumisha.”

Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Imepokelewa katika Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba pale muadhini anaposema:

قد قامت الصلاة

“Swalah imesimama.”

Akasema:

أقامها الله وأدامها

“Allaah aisimamishe na kuidumisha.”[1]

Lakini Hadiyth ni dhaifu haijengewi hoja.

[1] Abu Daawuud (01/411) na al-Baghawiy katika ”Sharh-us-Sunnah” (02/288). Haafidhw amesema katika “at-Talkhiysw” (01/211) amesema:

“Dhaifu.”

Ni dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “al-Irwaa´” (01/258).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 287
  • Imechapishwa: 04/05/2020