Hukumu ya manii na madhiy


Swali: Ipi hukumu ya madhiy yakiingia kwenye nguo, yaoshwe au yanyunyuziwe maji na kusafisha?

Jibu: Madhiy ni najisi, lakini najisi yake ni khafifu. Akinyunyuzia maji kwenye nguo yake, yatosha. Ama manii, ambayo ndio asli ya binaadamu, yanayotoka kwa nguvu na kwa shahawa na ladha, haya ni twahara. Yakiingia kwenye nguo au mwili, utatwahirisha. Lakini, kuifanya nguo ikawa safi au kuiosha kabisa ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaa ad-Darb (770) http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=8177
  • Imechapishwa: 29/12/2017